Kocha wa Yanga amewaaga wanajangwani leo.
Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa
timu ya Young Africans leo amewaaga rasmi wachezaji wake, viongozi, wapenzi
na wanachama baada ya kumalizaa wake wa miezi sita na sasa anakwenda
kujiunga na timu Al Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi Arabia,Imeripotiwa na mtandao wa Yanga.
Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza
Young Africans kwa kipindi cha miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti
aliyokua akiipata kutoka kwa wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu
hii kwa kipindi chote alipokuwa nchini Tanzania.
"Najua wengi itawashangaza
kuona naondoka lakini ukweli ni kwamba niikua na hiyo deal hata hata kabla ya
kuja Yanga, nilikua na makubaliano na timu ya Al Shoalah FCmakubaliano ambayo
yanaanza mwezi ujao hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi
kwa kipindi cha miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya
mkataba huo kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema
Hans
Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu
kuomba uanachama hivyo mimi ni sehemu ya Yanga na katika usajili ujao
nitawasaidia kuleta wachezaji wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu ujao
kwa Ligi ya Vodacom na mashindao ya Kimataifa.
Kocha Hans anaondoka leo nakwenda
Ghana kisha baadae atakwenda nchini Saudu Arabia tayari kwa kujiandaa na
maandalizi ya msimu ujao katika timu yangu hiyo ambayo nitaitumikia kwa kipindi
cha mwaka mmoja.
Kuhusu usajili kocha mkuu
ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha
baadae itawekwa wazi.
0 comments:
Post a Comment