Mwaikimba asema usingizi wake haupotezwi na Kavumbagu.
Mshambuliaji ngongoti wa Azam FC,
Gaudence Mwaikimba, amesema usajili wa Mrundi Didier Kavumbagu haumnyimi
usingizi hata kidogo kwani yeye ni mchezaji na anaijua kazi yake,imeripotiwa na Mwanaspoti.
Mapema wiki iliyopita, Azam
ilimsainisha Kavumbagu mkataba wa mwaka mmoja kutoka Yanga, hivyo kuongeza
ushindani wa namba kwenye safu ya ushambuliaji inayoundwa na washambuliaji;
Kipre Tchetche, John Bocco, Brian Umony na Gaudence Mwaikimba.
Mwaikimba ambaye hata kabla ya ujio
wa Kavumbagu hakuwa akipata nafasi kikosi cha kwanza licha ya kuchezeshwa
kwenye mechi za mwishoni msimu uliopita, alisema ujio wa Kavumbagu utawaongezea
nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na yeye binafsi anaamini bado ana nafasi ya
kukitumikia kikosi hicho.
“Kavumbagu ni mchezaji mzuri na
hakuna mtu asiyejua uwezo wake hivyo mimi binafsi nimefurahi kwa sababu ni
maendeleo kwenye timu hususani tunapojiandaa na maandalizi ya mechi za
kimataifa mwakani,” alisema Mwaikimba aliyewahi kukipiga Yanga miaka ya nyuma.
“Lakini mchezaji mahiri siku zote
haogopi ujio wa mchezaji mwingine, mimi ni mchezaji na ninaifahamu kazi yangu,
nitajitahidi kufanya vizuri ili kushindana.”
Chanzo:Mwanaspoti.
0 comments:
Post a Comment