TAIFA STARS NA ZIMBABWE KUCHEZA MBEYA MEI 18
MCHEZO wa
kwanza wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya Fainali
za Mataifa ya Afrika Morocco 2015 baina ya wenyeji Tanzania dhidi ya Zimbabwe
unaweza kufanyika mjini Mbeya, Mei 18, mwaka huu, imefahamika.
Katibu wa
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye
jana alikuwa mjini Mbeya kuukagua Uwanja wa Sokoine kama unakidhi sifa za
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) za mechi za kimataifa na inasemekana ripoti
yake ni nzuri.
Tanzania, au
Taifa Stars ilicheza mchezo wa kirafiki na Malawi kwenye Uwanja huo Mei 4,
mwaka huu na kwa namna ambavyo mashabiki wa soka mjini Mbeya waliisapoti timu
yao ya taifa, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi alitamani
timu hiyo icheze tena kwenye Uwanja huo.
Na kutokana na
mechi za Stars hivi sasa kukosa mvuto Dar es Salaam kwa sababu ya matokeo
mabaya, hata wachezaji wamependa kucheza mechi zao mikoani na Mbeya wameona
panafaa kuanzia.
Wakati wowote
kuanzia sasa TFF inatarajiwa kutoa tamko rasmi kuhusu mchezo huo kwamba
utafanyika Mbeya, au sehemu nyingine.
Tanzania
ikifanikiwa kuitoa Zimbabwe itamenyana na mshindi baina ya Msumbiji na Sudan
Kusini kuwania kuingia katika hatua ya makundi.
Na ikifuzu hapo
itaingizwa Kundi F pamoja na Zambia, Cerpe Verde na Niger kuwania kwenda
Morocco 2015.
0 comments:
Post a Comment