Breaking news;Diego Costa afuzu vipimo vya Afya Chelsea
Mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid ya Hispania, Diego Costa amefuzu vipimo vya afya Chelsea kuelekea uhamisho wake Pauni Milioni 32 kutoka Atletico Madrid,kwa mujibu wa Vyombo vya habari vya Uingereza.Kwa upande wa BBC na The Guardian wameandika jioni hii kwamba, Chelsea imefika bei ya manunuzi ya mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 25 wa Atletico na sasa wataingia kwenye mjadala wa vipengele binafsi
Mzaliwa huyo wa Brazil yumo kwenye kikosi cha Hispania kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil lakini kwa sasa kikosi kipo nchini Marekani.
Costa amefunga mabao 36 katika mechi 52 alizoichezea Atletico msimu huu ikitwaa ubingwa wa Hispania, La Liga kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996 na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kule Lisbon. na walifungwa mabao 4-1 na Madrid.
Costa atakumbukwa na Chelsea baada ya kufunga bao la pelnti pale Atletico ilipoichapa Chelsea 3-1 katika nusu fainali ya UEFA katika uwanja wa Stamford Bridge.
Costa alianza kucheza soka Ulaya katika klabu ya Ureno ya Sporting Braga na kujiunga na Atletico Mwaka 2007.
Baada ya kupelekwa kwa mkopo Celta Vigona Albacete na msimu moja Real Valladolid, akarudi tena ndani ya Atletico mwaka 2010,na pia akaitumikia Rayo Vallecano kwa mkopo mapema mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment