Polisi Tabora na Rhino kupambana leo,Mwadui na Kanembwa ligi daraja la kwanza.
Ligi daraja la kwanza itaendelea kunguruma leo ambapo Timu za Polisi Tabora na Rhino Rangers zitapambana katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi na nusu jioni huku Timu zote zikiahidi ushindi.
Kocha mkuu wa Rhino Rangers Bakari Best amesema kuwa mchezo huo utakuwa wa ushindani huku wao wakihitaji kushika nafasi za juu.
Best amesema kuwa hali ya timu ni nzuri ingawa mchezo wa mwisho walifungwa mabao 2-0 na Mwadui ya Shinyanga na kuongeza kuwa timu bado ina ari kubwa.
Naye Bernard Adam kocha msaidizi wa Polisi Tabora ameeleza kuwa timu ina ari kubwa huku mchezo wa mwisho walishinda mabao 2-1 dhidi ya Geita Sports.
Bernard amesema kuwa hakuna mchezaji ambaye anaumwa kwa hiyo mashabiki wa Polisi wategemee ushindi.
Mchezo huo ambao umevuta hisia za washabiki wengi utakuwa mgumu kwa pande zote
Vilevile Mwadui FC watawafuata maafande wa JKT Kanembwa ya Kigoma mjini Kigoma wakati Toto African watakuwa nyumbani jijini Mwanza kuvaana na timu ya maafande wa Polisi Mara.
Michezo mingine, Geita Gold watawafuata Green Warriors kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, JKT Oljoro watapepetana na jirani zao, Panone F.C na Burkina Faso ya Morogoro watakuwa wenyeji wa Polisi Dodoma.
Kundi B linaongozwa na Mwadui FC ambayo ina alama 36 ikifuatiwa na Toto alama 36,JKT Oljoro ina alama 29, Polisi Tabora alama 29 na Rhino alama 25.
0 comments:
Post a Comment