TFF yasema Polisi Tabora haina chake,Suala la Mbogo lapelekwa Bodi ya ligi.
Ombi la klabu ya Polisi Tabora FC kutaka mechi yao dhidi ya Toto Africans FC irudiwe kwenye uwanja huru (neutral ground) kwa madai ya kuchezeshwa zaidi ya muda unaotakiwa, na kutokuwepo ulinzi wa kutosha kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekataliwa.Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu za Mwadui FC na Polisi Mara FC dhidi ya Toto Africans kwa kumchezesha mchezaji Ladislaus Mbogo bila kuonyesha leseni yake yasikilizwe haraka na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa vile si ya kinidhamu.
Wakati huo huo, Kamati ya Nidhamu inaendelea na kikao chake leo (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko mengine ya kinidhamu yaliyofikishwa mbele yake.
0 comments:
Post a Comment