Viwanja 12 vya kombe la dunia Brazil 2014
Mechi ya fainali ya Kombe la Dunia
nchini Brazil itapigwa kwenye Uwanja wa Maracana, Julai 13, 2014.
Lakini, uwanja huo wa kihistoria ni
moja ya viwanja 12 katika miji 12 tofauti itakayotumika kwa ajili ya fainali hizo
za soka zitakazoshuhudia timu 32 zikimsaka mbabe mmoja wa Dunia.
Sports4lifetz inakupatia viwanja vyote 12 vitakavyotumika kwenye
fainali hizo za Kombe la Dunia ambazo zitaanza rasmi Juni 12 mwakani kwa mechi
ya Brazil dhidi ya Croatia itakayopigwa kwenye Uwanja wa Arena Corinthians jijini Sao Paulo.
1.Uwanja: Maracana Jiji: Rio de
Janeiro Uwezo: Watazamaji 73,531
Rio de Janeiro ni jiji la aina yake
Brazil na hakika Uwanja wa Maracana una historia ya kipekee katika soka la
Dunia. Maracana ilijengwa upya kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Ulifunguliwa Juni mwaka huu kwa mechi ya kirafiki kati ya Brazil na England.
Ndiyo uwanja utakaotumika kwa
fainali Julai 13 , mandhari yake nzuri ndicho kitu kinachovutia zaidi kwenye
mji huo kutokana na kuwa na fukwe safi na vivutio vingine vya kitalii kama
Mlima wa Sugar Loaf na Sanamu ya Christ the Redeemer.
Maracana ulitumiwa kwenye mechi ya
fainali ya Kombe la Dunia 1930, ambapo mashabiki 200,000 waliingia na
kuishuhudia Uruguay ikiichapa Brazil
2.Uwanja: Arena Corinthians uko Jijini Sao Paulo
una Uwezo: Watazamaji 65,000
Sao Paulo ni mji unaosifika kuwa
ndipo soka ilipozaliwa kwa nchi ya Brazil, lakini hali ya hewa yake imekuwa
tatizo kidogo.
Mji huo wa Kusini Mashariki
unafahamika kama Terra da Garoa kutokana na mvua kunyesha mara kwa mara.
3. Uwanja: Estadio Nacional
Mane Garrincha Jiji: Brasilia Uwezo: Watazamaji 68,009
Jina la uwanja huo limetokana na
nyota wa zamani wa Botafogo na Brazil, Garrincha, ambaye alikuwa mmoja wa
wanasoka mahiri kabisa nchini huko katika miaka ya 1950 na 1960.
Uwanja huo mpya ulitumika kwenye
mechi ya ufunguzi ya Kombe la Mabara. Brasilia ni jiji lenye wasanifu wengi wa
miundombinu. Ulianza kutambulika kama mji mkuu wa Brazil badala ya Rio de
Janeiro mwaka 1960.
4. Uwanja:
Estadio Castelao Jiji: Fortaleza Uwezo: Watazamaji 58,704
Uwanja huo ambao utatumika kwa mechi
ya pili ya Brazil ya hatua ya makundi umeandaliwa kwa kipindi cha miaka miwili
kwa ajili ya kutumika kwa fainali hizo za Kombe la Dunia. Fortaleza, mji uliopo
Kaskazini Mashariki mwa Brazil ni mjii wa mkuu wa kitongoji cha Ceara.
Fortaleza ni maarufu kwa utalii,
fukwe nzuri na vyakula vya aina yake na unatajwa kuwa na hali ya Kitropiki.
5. Uwanja: Estadio
Mineirao Jiji: Belo Horizonte
Uwezo: 57,483
Ni uwanja utakaotumika kwa mechi ya
nusu fainali na ni uwanja uliokamilika kwa wakati mara tu Brazil ilipotajwa
kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2014.
Straika wa zamani wa Brazil, Ronaldo
aling’ara kwenye uwanja huo wa Mineirao wakati alipoanza soka lake katika Klabu
ya Cruzeiro.
Upo umbali wa mwendo wa saa moja
kutoka Rio de Janeiro na ni mji usio na gharama kubwa kwa mashabiki wa kigeni.
6. Uwanja: Estadio
Beira-Rio
Jiji: Porto Alegre
Uwezo: 48,849)
Uwanja huo upo kando ya Mto Guaiba.
Unatumika kama uwanja wa nyumbani wa klabu mbili maarufu za Internacional na
majirani zao Gremio. Porto Alegre ni mji wenye mvua kipindi cha Juni na Julai
na visiwa na kimojawapo ni Lago de Patos kilichozungukwa na miti karibu milioni
moja.
7.Uwanja: Arena Pernambuco
Jiji: Recife
Uwezo: Watazamaji 44,248
Jiji la Recife, lipo kwenye Pwani ya
Kaskazini Mashariki ya Brazil, ulitumika mara ya mwisho katika mechi ya Kombe
la Dunia 1950. Kwa sasa umejengwa upya na unatumiwa na klabu tatu zenye
historia ya kipekee Brazil za Nautico, Santa Cruz na Sport. Wakazi wake ni
vichaa wa soka.
Recife ni mji mkuu wa Pernambuco ni
muhimu sana kwa uchumi wa Brazil.
8.Uwanja: Arena Fonte Nova
Jiji: Salvador
Uwezo: Watazamaji 52,048
Uwanja huo utashuhudia mechi sita
kwenye fainali hizo. Waandaaji wanasema uwanja huo mpya umejengwa kisasa na una
migahawa, makumbusho za soka, maduka, hoteli na kumbi za sherehe.
9. Uwanja:
Arena Pantanal
Jiji: Cuiaba
Uwezo: Watazamaji 42,968
Uwanja huo uliboreshwa kwa ajili ya
fainali za Kombe la Dunia na utatumika kwa ajili ya mechi nne. Uwanja huo upo kwenye
mji wa Cuiaba uliopo Magharibi mwa Brazil, Kusini mwa misitu ya Amazon.
Mji
huo unafahamika kama ‘Green City’
na ni maarufu kwa utalii licha ya kwamba kwa kipindi cha Juni hadi Julai hali
ya hewa inakuwa tatizo kutokana na joto kufikia nyuzi 40.
10. Uwanja:
Arena Amazonia
Jiji: Manaus
Uwezo: Watazamaji 42,374
Kama jina la uwanja huo
linavyosomeka, Manaus ipo katikati ya misitu ya Amazon. Manaus si mahali pazuri
sana kwa soka, lakini waandaaji wa Kombe la Dunia waliamua michuano hiyo
ifanyike kila kona ya nchi ya Brazil licha ya kwamba uwanja huo unaweza kuwa
bustani ya wanyama michuano itakapokwisha.
11. Uwanja: Estadio das Dunas
Jiji: Natal
Uwezo: Watazamaji 42,086
Uwanja huo umemalizika kujengwa kwa
ajili ya Kombe la Dunia. Estadio das Dunas utatumika kwa mechi nne za makundi
katika fainali hizo. Natal ni mji unaofahamika kama Cidade do Sol (Sun City)
kwa sababu umekuwa na joto linalokaribia nyuzi 28. Fukwe zilizopo Kaskazini
Mashariki mwa jiji hilo zinaifanya jiji hilo lizidi kupendeza.
12. Uwanja: Arena da Baixada
Jiji: Curitiba
Uwezo: Watazamaji 41,456
Uwanja huo wa Arena da Baixada kwa mara
ya kwanza ulijengwa 1914, lakini ulifanyiwa ukarabati mwaka 1999 na
ulirekebishwa zaidi baada ya Brazil kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa fainali za
Kombe la Dunia 2014.
Curitiba ni mji wa aina yake ndani
ya Brazil na unatajwa kuwa na uchumi mkubwa. Hali yake ya hewa inafanana na Rio
de Janeiro na Belo Horizonte.
0 comments:
Post a Comment