Valverde amsubiri kwa hamu Dembele
Kocha mkuu wa Barcelona Ernesto Valverde amesema kuwa Ousmane Dembele ataleta mafanikio ndani ya klabu yake.
Jana mchana kuwa Barcelona walikuwa wameshafikia makubaliano ya dili la paundi milioni 96.8 na Borussia Dortmund kwa ajili ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa mchezaji ghali zaidi wa pili duniani.
Mshambuliaji huyo amefunga mara 10 na kutoa pasi za mabao 18 katika mechi 47 alizocheza Dortmund msimu wa 2016-17, na Valverde amebainisha kuwa uzalendo unamshinda kuendelea kusubiri mchezaji huyo kutua Camp Nou.
Barcelona wataendelea na kampeni za La Liga 2017-18 kucheza dhidi ya Alaves Jumamosi usiku.
Ousmane Dembele anatarajiwa kutua Barcelona Jumapili na Jumatatu atafanyiwa vipimo kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano Camp Nou.
0 comments:
Post a Comment