Baada ya mashabiki kuanza kukoroma,Pardew awajibu
Kocha wa klabu ya
Newcastle United, Alan Pardew bado anaamini anaweza kubakia kwa muda mrefu
kuifundisha timu hiyo pamoja na kupoteza mechi sita mfululizo na kusababisha
mashabiki kuchukizwa.
Mashabiki hao wa
Newcastle wameonyesha hasira zao kufuatia kipigo cha mabao 3-0 walichopata
kutoka kwa Arsenal jana usiku.
Akihojiwa Pardew amesema
anajua mashabiki hao wamehuzunishwa na kukasirishwa hivi sasa kwasababu
hawajapa matokeo mazuri lakini ameomba uvumilivu kwani ana mipango ya muda
mrefu na timu hiyo.
Newcastle walianza
vyema msimu mpaka kumalizika kwa mzunguko wa kwanza lakini walionekana
kuporomoka toka kuanza kwa mwaka huu mpaka kufikia nafasi ya nane waliyopo hivi
sasa.
0 comments:
Post a Comment