Monday, 6 April 2015

VPL Mtibwa yasukumwa na Stendi hadi mstari wa kushuka daraja.

Klabu ya Stand United ya Shinyanga imefanikiwa kushinda bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwa siku mbili kuanzia hapo jana na leo.

Bao la Stand United lilifungwa jana na Haruna Chonongo katika dakika ya 12 kabla ya pambano hilo kuvunjika dakika ya 33 kufuatia mvua kubwa kunyesha mjini Shinyanga.

Mchezo huo ulichezeshwa kwa dakika 57 zilizosalia asubuhi na mechi kumalizika kwa 0-0.

Kwa matokeo hayo Stand United wanafikisha alama 24, alama moja mbele ya Mtibwa wenye alama 23 na kuwafanya Mtibwa kushikilia nafasi ya 12 kati ya timu 14 zinazoshiriki ligi ya VPL.

Ligi hiyo itaendelea kunguruma jioni kwa mchezo moja kupigwa uwanja huo wa Kambarage ambapo wenyeji Kagera Suukari wanachuana na Simba SC.

Awali mechi hiyo ilitakiwa kupigwa jumamosi iliyopita, lakini iliahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji kutokana na mvula zinazoendelea kunyesha.

0 comments:

Post a Comment