Saturday, 17 May 2014

Mashindano ya vyuo Tabora kesho fainali ni UHAZILI na NYUKI

Mashindano ya vyuo mkoani Tabora yamefikia hatua ya fainali ambapo chuo cha Uhazili kitapambana na chuo cha Nyuki Siku ya kesho jumapili Mei 18,2014. 
Mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Mwinyi umefika hatua hiyo wakati Uhazil iliwatoa chuo cha Tumbi kwa ushindi wa 1-0 ilhali timu ya Amucta au SAUT Iliwapa fursa Nyuki kutinga fainali baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali. 
Mashindano hayo ya vyuo yalianza Mei 5 2014 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na yalikuwa katika makundi mawili ya A na B ambapo kundi la A iliundwa na timu za Tumbi,Amucta na Veta wakati kundi la B iliundwa na Nyuki,Uhazili na Teku. 
Tumbi na Amucta walifuzu kwenda nusu fainali kama washindi wa kwanza na wa pili wakati Nyuki na Uhazili ni washindi wa kundi hilo la B. 
Mtandao huu ulikwepo katika hatua ya mwanzo mpaka sasa na inakupatia historia ya timu zote zilizofika fainali.
Uhazili ilifika fainali baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza mei 6 dhidi ya TEKU kwa mabao 2-1 lakini katika mchezo wa pili mei 8 walifungwa bao 1-0 na Nyuki na kutinga katika hatua hiyo kama washindi wa pili  huku Nyuki wakiongoza kundi hilo kwa mantiki hiyo timu zote zinazocheza fainali zimetoka kundi la B.
Safari ya Uhazili kutinga fainali iliendelea pale walipoichapa Tumbi bao 1-0
Nyuki walianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uhazili  mei 8 katika kundi hilo la B na mchezo wa pili walishinda bao 1-0 dhidi ya TEKU pale mei 10.Nyuki walitinga nusu fainali wakiwa kinara wa kundi hilo na walicheza na Amucta na kushinda mabao 2-1.
Jumapili  vijana hao waliotoka kundi moja watapambana huku Nyuki kupitia kocha wao wakisema kuwa wataendeleza rekodi yao ya kushinda na kubeba kombe hilo.
Amucta na Tumbi watacheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu siku hiyohiyo ya jumapili.

0 comments:

Post a Comment