Ngorongoro Heroes kuondoka kesho kuelekea Nigeria
KIKOSI
cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda
Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi Mei 24 mwaka huu katika Jiji la Kaduna kwenye
Jimbo la Kaduna ambalo lipo
katikati ya Nigeria.
Msafara
wa timu hiyo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Ngorongoro Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0
Ngorongoro Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0
Mwamuzi
Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye
atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na
Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.
0 comments:
Post a Comment