Wednesday, 21 May 2014

Pique ajifunga zaidi Barcelona,Sagna kuelekea Manchester city.

Usajili barani Ulaya umeendelea kuchukua nafasi yake ambapo hii leo  kipa mkongwe wa AC  Milan Christian Abbiati (pichani) ameongeza mkataba wa kuidakia klabu hiyo hadi mwakani Juni 30.
Wakati jana Gerard Pique wa Barcelona ameongeza mkataba wa kuichezea klabu hiyo hadi mwaka 2019.
Beki wa kulia wa Arsenal,Bacary Sagna anajiandaa kusaini mkataba na Manchester City ambao utamfanya awe analipwa kiasi cha pauni laki 1 na efu 40 kwa wiki( £140,000).
Mfaransa huyo anamaliza mkataba na washika bunduki na alionyesha dhairi kutotaka kuendelea kusalia Emirates Stadium.
Klabu za Liverpool na Newcastle United zipo katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa West Ham,Mohamed Diame
Arsene Wenger anajiandaa kumnyakua beki wa Toulouse,Serge Aurier ambapo ndiyo utakuwa uhamisho wake wa kwanza kipindi hiki cha majira ya joto ili akazibe nafasi ya Bacary Sagna ambaye anataraji kujiunga na Manchester City mara baada ya kombe la dunia.
Klabu ya Valencia ipo njiani kutafuta mshambuliaji mpya majira ya joto na tayari wameonyesha nia ya kumtaka nyota wa Benfica,Rodrigo
Newcastle wana dhumuni la kupeleka ofa kwa kiungo wa Montpellier,Remy Cabella kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia.
Nyota huyo mwenye miaka 25 yupo katika orodha ya wachezaji wanaoweza kuitwa baadae kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa na thamani yake inafikia Euro milioni 10 huku Newcastle wakiwa wameandaa ofa ya Euro milioni 8.
Inter Milan wanatazamia uwezekano wa kumnasa mchezaji wa Borussia Monchengladbach,Granit Xhaka majira haya ya joto wakiwa na lengo la kuimarisha safu yao ya kiungo.
Roma wapo katika hali ya kumtaka winga wa Porto,Juan Iturbe ambaye alicheza msimu wa mwaka 2013-14 kwa mkopo katika klabu ya Verona na itawalazimu watoe kiasi cha Euro milioni 15 kwa nyota huyo
Manchester City na Newcastle United zimekiri kuwa katika mbio za kutaka kupata saini ya beki wa kati wa Stoke City,Ryan Shawcross.
ia Everton anajiandaa kumbakiza Lacina Traore kwa mkopo wa muda mrefu zaidi klabuni hapo mara baada ya kumchukua mwezi Januari kutoka katika klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Imeandaliwa na mtandao huu kushirikiana na mitandao ya nje.

0 comments:

Post a Comment