Taifa stars uso kwa uso na Zimbabwe hii leo
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itapepetana na Zimbabwe maarufu kama Mighty Warriors hii leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON 2015 kule nchini Morocco.
Kuelekea mchezo huo wachezaji wawili wanochezea klabu ya TP Mazembe Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamewasilini nchini jana jumamosi tayari kwa ajili ya mpambano huo.
Mshindi kati ya Zimbabwe na Stars atacheza na mshindi kati ya Msumbiji au Sudan kusini na baada ya hapo atapangwa kundi la F tayari kwa kuanza hatua ya makundi.
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema
kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, kwani kimepata mechi
za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye kambi iliyoanzia Tukuyu mkoani
Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.
Naye Kocha Msaidizi wa Zimbabwe, Kalisto
Pasuwa amesema hawaifahamu vizuri Taifa Stars lakini wamekuja kwenye
mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa ajili ya kushinda, na kuwataka
washabiki wajitokeze kwa wingi kuona kiwango cha timu yake.
Milango kwa ajili ya mechi hiyo
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana wakiongozwa na Joseph Odartei
Lamptey itakuwa wazi kuanzia saa 6 kamili mchana, na tiketi zitapatikana
katika magari maalumu uwanjani hapo.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000
kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu, sh. 10,000 kwa VIP C na
B, na sh. 20,000 kwa VIP A.
0 comments:
Post a Comment