Monday, 16 June 2014

Klose akifunga bao moja leo ataifikia rekodi ya Ronaldo

Michezo ya kombe la dunia inaingia siku yake ya 5 huku dunia leo ikisubiri mchezaji mkongwe wa Ujerumani Miroslav Klose kusawazisha rekodi ya ufungaji mabao tokea kombe la dunia lianze mwaka 1930 iwapo akifunga bao na itategemea kama akipangwa na kocha  Joachim Loew katika mchezo utakaopigwa hapo baadaye Ujerumani na Ureno.
Klose, mwenye miaka 36 mchezaji wa kihistoria aliyefunga mabao mengi kwa upande wa Ujerumani amefunga mabao 14 nyuma ya mshambuliaji hatari enzi hizo wa Brazil  Ronaldo Nazario de Lima mwenye mabao 15 ya kombe la dunia.                         Wachezaji waliofunga mabao mengi kombe la  dunia
   Mchezaji/Nchi     Mabao   
Ronaldo-Brazil 15
Miroslav Klose-Ujerumani 14 
Gerd Muller-Ujerumani 14 
 Just Fontaine-Ufaransa 13
 Pele-Brazil 12 
 Sandor Kocsis-Hungary 11 
 Jurgen Klinsmann-Ujerumani 11 
 Helmut Rahn-Ujerumani 10 
 Gary Lineker-uingereza 10 
 Gabriel Batistuta-Argentina 10 
Akizungumzia mchezo huo wa hapo baadaye kocha  Loew ameeleza kuwa atafurahi iwapo Klose akifunga lakini akasisitiza kuwa acheze na si kuangalia rekodi
"Iwapo  Miroslav atacheza katika kikosi cha kwanza au akitokea benchi kwetu ni mchezaji muhimu sana,mchezaji wa kuigwa ndani na nje ya uwanja." alisema Loew
Wenye mabao mengi kombe la dunia
Klose anaweza kuanzia benchi huku Thomas Mueller akipewa nafasi kubwa
Klose alivunja rekodi ya baba yake na Thomas Muller yaani Gerd Mueller ya kuwa mfungaji bora wa Ujerumani kwa miaka  40 baada ya kufikisha mabao  69 wakati Armenia ikifungwa mabao 6-1 na Ujerumani mchezo wa kirafiki.
Mchezo wa leo utaanza saa moja kamili usiku wa leo.
Akiwa amecheza michezo  19 ya kombe la dunias, Klose  anaweza kufikia rekodi ya  Lothar Matthaeus aliyecheza mechi  25 lakini itategemea na mwenendo wa Ujerumani katika mashindano ya mwaka huu labda ifike hatua ya Nusu au fainali.

0 comments:

Post a Comment