Thursday, 5 June 2014

Victoria University mabingwa wa CECAFA Nile Basin

Klabu ya Victoria University  ndio Mabingwa wa Mashindano mapya ya CECAFA NILE BASIN  baada kuichapa AFC Leopards ya Kenya mabao 2-1 katika Fainali iliyochezwa huko Khartoum International Stadium Jijini Khartoum Nchini Sudan hapo Jana.
Haya ni Mashindano ya kwanza kabisa ya Kombe hilo yaliyoshindaniwa na Klabu kadhaa kutoka Nchi za Afrika Mashariki na ya Kati ambao ni Wanachama wa CECAFA.
Kwa ushindi huo, Victoria University pia wamejinyakulia Donge nono la Dola 30,000 na ni baraka kwa Klabu changa iliyoshiriki michuano ya CECAFA kwa mara ya kwanza kabisa.
Victoria University ndio waliowatoa Wawakilishi wa Tanzania Bara, Mbeya City, kwenye Robo Fainali baada ya kuwafunga Bao 1-0 kwa Bao la Penati.
Kwa kuwa Washindi wa Pili, AFC Leopards walipewa Dola 20,000.

0 comments:

Post a Comment