Real Madrid watulizwa na Athletico,Athletico mabingwa wa Super Cup
Mchezaji mpya aliyetokea Bayern Munich Mario Mandzukic ameipa ushindi klabu yake ya Atletico Madrid wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Real Madrid na kubeba Super Cup ya Hispania mchezo uliopigwa Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania.Bao la Raul Garcia katika mchezo wa kwanza kule Santiago Bernabeu uliisaidia Atletico kupata sare ya 1-1 na hivyo Athletico kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment