Saturday, 18 October 2014

VPL Simba na Yanga,Mbeya City na Azam leo.

Ligi kuu ya soka Tanzania Bara hii leo inaingia katika mechi ya nne huku wakongwe wa soka la Tanzania Simba na Yanga wakipambana.

Simba wao hawajafungwa lakini hawajashinda hata Mechi moja katika Mechi 3 walizocheza kwa kutoka Sare na 2-2 na Coastal Union na Sare za 1-1 dhidi ya Stand United na Polisi Morogoro.

Kwa upande wa Yanga walianza kwa kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro na kisha kushinda Mechi mbili mfululizo dhidi ya Ruvu JKT na Prisons, zote kwa mabao 2-1 kila moja.

Katikati ya uwanja mwamuzi atakuwa  Israel Nkongo ambaye atasaidiwa na Ferdinand Chacha na John Kanyenye wakati Hashim Abdallah atakuwa mwamuzi wa Akiba na Kamishna ni Salum Kikwamba.

RATIBA:

Jumamosi Oktoba 18

Polisi Moro v Mtibwa Sugar

Ndanda FC v Ruvu Shooting

Kagera Sugar v Stand United

Coastal Union v Mgambo JKT

Mbeya City v Azam FC

Yanga v Simba

Jumapili Oktoba 19

Prisons v JKT Ruvu

0 comments:

Post a Comment