Aliyechezesha Yanga na Ruvu Shooting aondolewa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Chama, mwamuzi huyo Mohammed Theofil ameondolewa kuchezesha ligi hiyo ya Tanzania Bara kwa kipindi kilichobaki.
Chama ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Katibu wa Chama cha Soka Kagera, alithibitisha kuondolewa kwa mwamuzi Theofil.
Aidha amesema kuwa Tarehe sita mwezi ujao, Kamati (ya Waamuzi) itakutana na kupitia CD ya mchezo pamoja na taarifa ya Kamisaa wa mchezo huo na kuchukua hatua zaidi kwa mwamuzi kama itaonekana anastahili adhabu zaidi.
Alisema kwa sasa wamechukua hatua ya kumwondoa katika kuchezesha Ligi Kuu kwa sababu katika ratiba yao mpya kwa mechi zijazo za Ligi Kuu, mwamuzi huyo alikuwa amepangwa kuchezesha mechi nne, hivyo wameona si vyema kumwacha aendelee kuchezesha mechi zaidi.
0 comments:
Post a Comment