Thursday, 5 February 2015

Nchi tano zathibitisha kushiriki Judo

Nchi tano zimethibitisha ushiriki wake kwenye mashindano ya Judo ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kufanyika kuanzia wiki ijayo, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA) ,Innocent Mallya, maandalizi kuelekea kwenye michuano hiyo yamekamilika na lengo lao kwa upande wa Tanzania ni kuendelea kutetea ubingwa.

Mallya alisema mashindano hayo yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi (CCP) yatashirikisha timu kutoka Kenya, Burundi, Rwanda, Ehiopia, Zanzibar na Tanzania bara.

Mallya amesema Mambo yamekamilika na wana  imani mashindano yataenda vizuri kinachohitajika ni mashabiki wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo utakaokuwa na upinzani mkali.

Alisema kwa upande wa Tanzania ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, wamejiandaa vizuri na wanategemea kuwa tena bingwa.

Alisema iwapo watafanikiwa kufanya vizuri, baadaye watachaguliwa wachezaji watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya Afrika ‘All African Game’ itakayofanyika Septemba mwaka huu, Kinshansa, Congo na kwenye michezo ya Olimpiki mwakani.

Mallya alisema mchezo huo hautakuwa na kiingilio na kwamba washiriki watakuwa 103 kutoka katika nchi hizo. Mashindano hayo kwa mwaka jana yalifanyika Kenya na sasa ni zamu ya Tanzania.

Chanzo Habari leo.

0 comments:

Post a Comment