Thursday, 5 February 2015

Kocha wa Ivory Coast asema wamecheza vibaya ingawa wameshinda.

Kocha mkuu wa Ivory Coast , HERVE RENARD amesema kikosi chake hakikucheza kwa kiwango kizuri licha ya kuibuka  na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya KONGO,usiku wa kuamkia leo.

Tembo walitinga fainali ya AFCON baada ya nahodha YAYA TOURE kuwafungia bao la kuongoza katika dakika ya 20, lakini DR Congo wakasawazisha dakika 3 baadaye kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na  DIEUMERCI MBOKANI.

GERVINHO aliifungia Ivory Coast dakika nne kabla ya mapumziko na  WILFRIED KANON alifunga bao la ushindi katika dakika ya 68.

Kocha huyo amesema "Sikupenda mchezo huu. Tulicheza kirahisi sana na hatukuwaheshimu wapinzani wetu ambao walitoka nyuma na kuifunga Congo Brazzaville hatua ya robo fainali," Amesema Renard.

"Hatukuonesha malengo ya kutosha-labda mashabiki wachache waliohudhuria hawakutupa shangwe za kutosha"

"DR Congo siku zote ni timu hatari. Walikuwa haraka kufanya mashambulizi ya kushutukiza wakimtumia Mbokani na (Yannick).

"Lakini kitu muhimu ni kwamba tupo fainali na tuna matumaini ya kurudisha kombe Abidjan. Alimaliza kwa kusema hivyo  Renard.

Ivory coast itacheza fainali huku ikimsubiri mshindi wa leo ambapo Wenyeji GUINEA YA IKWETA watapambana na  GHANA.

0 comments:

Post a Comment