Polisi Tabora kuwavaa Polisi Mara FDL
Msafara wa wachezaji na viongozi 30 wa Klabu ya POLISI TABORA umeondoka leo asubuhi kuelekea mkoani Mara kwa ajili ya mpambano wa ligi daraja la kwanza dhidi ya POLISI MARA.Mpambano huo utapigwa keshokutwa katika uwanja wa Karume mjini Musoma.
Msemaji wa Klabu hiyo Omar Matesa Amesema kwa maandalizi waliyoyafanya wana uhakika wataibuka na ushindi.
Matesa amesema kuwa jana walifanya maandalizi ya mwisho na mwalimu mkuu Kim Christopher na msaidizi wake Benard Fabian wameridhika na hali ya wachezaji.
POLISI TABORA imebakiwa na mechi tatu huku mechi mbili watacheza nje ya mkoa wa Tabora dhidi ya POLISI MARA NA MWADUI YA SHINYANGA na kucheza mchezo moja hapa TABORA dhidi ya JKT OLJORO YA ARUSHA.
Kwa sasa Polisi ina alama 35 na kushikilia nafasi ya nne katika kundi B linaloongozwa na Mwadui ambao wana alama 40 wakifuatiwa na Toto alama 39 huku Oljoro wana alama 38.
0 comments:
Post a Comment