Monday, 2 February 2015

"Timu bora imetolewa"-Renard

Kocha wa timu ya taifa ya IVORY COAST HERVE RENARD amesema timu bora kwenye michuano ya Mwaka huu ya kombe la mataifa ya AFRIKA imetolewa.

Kauli ya RENARD imekuja baada ya timu yake kuiondosha ALGERIA kwa magoli MATATU kwa moja hapo jana kwenye mechi ya robo fainali ya michuano hiyo.

Ushindi wa IVORY COAST hiyo jana umetokana na magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Wilfried Bony na moja likifungwa na Gervas Gervinho.

Baada ya Mchezo huo kocha HERVE RENARD amesema "Nafikiri Tumeifunga timu bora kwenye michuano hii.Tunahgitaji kujipanga vizuri sana ili tuweze kujaribu kupambana na timu yenye wachezaji” alisema Herve Renard.

Kama utakumbuka ni kocha huyu huyu RENARD aliyeiongoza ZAMBIA kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya AFRIKA Mwaka 2012.

Wakati Zambia wanatwaa ubingwa huo, IVORY COAST ndio iliyokuwa timu bora ya michuano hiyo Mwaka 2012, lakini hatimaye ZAMBIA ikashinda kwa mikwaju ya penati.

Kocha wa ALGERIA CHRISTIAN GOURCUFF amekubaliana na maoni ya kocha RENARD na hana malalamiko kuhusu namna timu yake ilicheza.

Kwa matokeo ya jana sasa tunasubiri mitanange ya nusu fainali kuanzia jumatano hii ambapo IVORY COAST itaivaa JAMUHURI YA KIDEMOKRASI YA CONGO na GHANA wakicheza siku ya ALHAMIS na wenyeji EQUATORIAL GUINEA

0 comments:

Post a Comment