Tuesday, 27 May 2014

Diego Costa hatihati kombe la dunia

Mshambuliaji aliyecheza dakika 9 mchezo wa fainali Ligi ya mabingwa Ulaya baina ya Athletico na Real Madrid  Diego Costa yuko hatarini ya kukosa Kombe la Dunia la mwezi ujao baada ya madaktari kuonya kwamba jeraha la msuli ya paja litamuweka nje wiki mbili,imelezwa na Supersports.com.
“Hayuko kwenye hali nzuri. Yuko kwenye hali sawa na aliyokuwa kabla ya mechi hiyo,” akasema Daktari Pedro Guillen, mkuu wa kliniki ya Cemtro ambapo Uhispania ilituma mchezaji huyo akachunguzwe.
“Ana jeraha la kiwango cha kwanza katika msuli wa paja lake la kulia na anahitaji kupumzika angalau wiki mbili,” daktari huyo aliambia kituo cha redio cha Cope.
Uhispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na dunia watacheza mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia ngazi ya makundi dhidi ya Uholanzi Juni 13.
“Anaweza kucheza, lakini hili litategemea na atakavyopiga hatua,” Guillen alisema.
Meneja wa Uhispania Vicente del Bosque ameahirisha kutajwa kwa kikosi chake kamili akisubiri kuona kama Costa atapona kabisa na pia akisubiri kuona hali ya wachezaji wa Atletico na Real Madrid baada ya fainali ya Jumamosi.
Real walishinda 4-1 kwenye pambano hilo Lisbon ambalo lilienda muda wa ziada.
Del Bosque alitaja mafowadi watatu – David Silva, Fernando Torres na Pedro Rodriguez – kwenye kikosi cha wachezaji 19 wa mechi ya kirafiki dhidi ya Bolivia Mei 30.
Atataja kikosi chake kamili cha Kombe la Dunia baada ya mechi hiyo, na anaweza kuongeza Costa na wachezaji wengine wa Atletico na Real Madrid kwenye orodha ndefu kabla ya kuwapunguza hadi 23.
Uhispania watakabili Chile na Australia katika Kundi B Kombe la Dunia pamoja na Uholanzi – waliokuwa wapinzani wao kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2010 ambayo waliibuka washindi.

0 comments:

Post a Comment