Tuesday, 27 May 2014

Kikosi cha Zambia chatajwa kucheza na Japan

Kocha wa timu ya taifa ya Zambia  Patrice Beaumelle  ametangaza kikosi  cha wachezaji ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Japan siku ya  June 6.
Beaumelle amewaita wachezaji watatu kutoka  kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20) ambacho kiliitoa timu ya  Msumbiji katika raundi ya pili ya kufuzu kwenda Senegal kwa michuano ya vijana  chini ya umri huo mwaka  2015.
Wachezaji hao ni viungo  Lubambo Musonda,mshambuliaji   Patrick Ngoma na kipa Mangani Banda.
Pia amewaita  Isaac Chansa, Mukuka Mulenga na  James Chamanga.

Mchezo huo utachezwa katika mji wa  Tampa, Florida  katika uwanja wa  Raymond James  kule Marekani.
Zambia  inajiandaa kwa ajili ya kufuzu mataifa Afrika lakini Japana wanatumia mchezo huo kwa ajili ya kuelekea kombe la dunia kule Brazil ambapo wamepangwa sambamba na Colombia, Greece na Ivory Coast katika kundi la C
Kikosi:
Makipa: Kennedy Mweene, Toaster Nsabata, Mangani Banda, Joshua Titima
Walinzi: Davies Nkausu, Jimmy Chisenga, Stoppila Sunzu, Hichani Himonde, Kondwani Mtonga, Joseph Musonda, Emmanuel Mbola, Rodrick Kabwe, Adrian Chama, George Chilufya
Viungo: Nathan Sinkala, Justin Zulu,Isaac Chansa, Chisamba Lungu, Felix Katongo, Christopher Katongo, Fwayo Tembo, Mukuka Mulenga, Lubambo Musonda, Shadreck Malambo, Kennedy Mudenda
Washambuliaji: Jacob Mulenga, Emmanuel Mayuka, Moses Phiri, Ngoma Patrick, James Chamanga

0 comments:

Post a Comment