Monday, 5 May 2014

La liga Ronaldo ainusuru Madrid

Mchezaji  bora wa dunia, Cristiano Aveiro dos Santos Ronaldo jana alifunga bao nzuri na kuinusuru Real Madrid kupoteza mechi.
Valencia ilionekana kubeba alama zote tatu Uwanja wa Santiago Bernabeu, lakini mshindi huyo wa Ballon d'Or aliinusuru timu yake tena, alipounganisha krosi ya Angel di Maria kwa utaalamu wa hali ya juu baada ya kuunganisha mpira huo kwa kisigino cha juu
Mathieu alianza kuifungia Valencia dakika ya 44, lakini Sergio Ramos akaisawazishia Real Madrid dakika ya 59 na Parejo akawafungia wageni bao la pili, kabla ya Ronaldo kufunga lake la 50 msimu huu.
Licha ya Atletico kufungwa 2-0 na Levante, bado ipo kileleni mwa La Liga kwa alama zake 88 za mechi 36, ikifuatiwa na Barcelona alama 85 mechi 36 wakati Real sasa ni ya tatu kwa alama zake 83 za mechi 35.

0 comments:

Post a Comment