Kikosi cha mwisho cha Argentina kuelekea Brazil.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Argentina, Alejandro Sabella, amepunguza Kikosi chake cha kwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia kutoka Wachezaji 30 kwa kuwaondoa Wachezaji wane.Kwenye Fainali zinazoanza Brazil hapo Juni 12, kila Timu inatakiwa iwasilishe Majina ya Wachezaji wao 23 wa mwisho kwa FIFA ifikapo Juni 2.
Wachezaji hao Wanne walioondolewa ni Franco Di Santo, aliewahi kuzichezea Wigan na Blackburn huko England na sasa yuko Werder Bremen, na wengine ni Kiungo wa Sporting Lisbon Fabian Rinaudo, Beki wa River Plate Gabriel Mercado na mlizi wa kati wa Benfica Lisandro Lopez.
Argentina, ambao walitwaa Kombe la Dunia Mwaka 1978 na 1986, wako KUNDI F pamoja na Bosnia, Nigeria na Iran.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Sergio Romero (Monaco), Mariano Andujar (Catania), Agustin Orion (Boca Juniors).MABEKI: Ezequiel Garay (Benfica), Federico Fernandez (Napoli), Pablo Zabaleta (Manchester City), Marcos Rojo (Sporting Lisbon), Jose-Maria Basanta (Monterrey), Hugo Campagnaro (Inter Milan), Nicolas Otamendi (Atletico Mineiro), Martin Demichelis (Manchester City).
VIUNGO: Fernando Gago (Boca Juniors), Lucas Biglia (Lazio), Javier Mascherano (Barcelona), Ever Banega (Newell's Old Boys), Angel Di Maria (Real Madrid), Maxi Rodriguez (Newell's Old Boys), Ricardo Alvarez (Inter Milan), Augusto Fernandez (Celta Vigo), Jose Sosa (Atletico Madrid), Enzo Perez (Benfica).
MAFOWADI: Sergio Aguero (Manchester City), Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Ezequiel Lavezzi (Paris St Germain), Rodrigo Palacio (Inter Milan)

0 comments:
Post a Comment