
Ligi mbalimbali duniani zimemalizika katika msimu wa mwaka 2013-2014 lakini kuna baadhi ya wachezaji wanavuta pesa ndefu ilhali timu zo zimepata nafasi za juu ama hata wengine kushindwa kuisaidia timu zao.
Hawa ni wachezaji 10 bora matajiri katika ligi kuu ya Uingereza
1.Wayne Rooney – £45m
Mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya Manchester United,anapata mshahara wa 250.000£ kwa wiki,mashabiki wengi wanaamini kuwa anaweza kustaafu akiwa na klabu hiyo ya Old Traford amabayo itanolewa na kocha mholanzi Van Gaal baada ya kombe la dunia,amesaini mkatba wa miaka mitatu.
2.Samuel Eto’o – £39m
Mchezaji tajiri kuliko wote anayetoka nje ya Uingereza,japo kwa sasa maelewano yake na kocha Mourinho si mazuri kutokana na hali ya kurushiana maneno na bosi huyo mbwatukaji.
3.Rio Ferdinand – £37m
Ametangaza kuikacha klabu yake ya Manchester United japo bado anashikilia nafasi ya 3,ana miliki kiasi cha 37milion paunds. Ila ametangaza kuachana na wababe hao ambao wameshindwa kufuzu mashindano ya Ulaya hapo mwakani japo mkataba wake unaisha mwaka huu.
4. Frank Lampard – £31m
Roho ya Chelsea Frank Lampard anashika nafasi ya 4 ana paundi mil
31 katika akaunti yake,ana miaka 35 na anaweza kusaini mkataba mwingine ndani ya Chelsea
5.John Terry – £29m
Wiki iliyopita alisaini makatba wa mwaka moja wa kuitumikia Chelsea,kwa wiki analipwa £150,000
6.Steven Gerrard – £29m
Mkongwe na nahodha wa Liverpool Steven Gerrard akiweza kusaini mkataba mwingine wa kuitumikia klabu hiyo na akistaafu Anfield atakuwa mchezaji tajiri kuliko wote kwa sasa ana utajiri wa paundi mil 29.
7. Ryan Giggs (Manchester United) £27m
Amestaafu rasmi soka mapema wiki hii,akiwa na umri wa miaka 40 na atakuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo.Amecheza michezo 963 akiwa na vikombe 34 na kufunga mabao 162.
8. Fernando Torres – £26m
Mhispania
Fernando Torres anachezea Chelsea bado hajaonyesha kiwango kizuri chenye ushawishi wa kutosha baada ya kusajiliwa 50.000£ akitokea Liverpool. Anashika nafasi ya 8,ana utajiri wa paundi mil 25.
9.Yaya Toure – £25m
Kwa sasa unaweza kusema kuwa ni kiungo bora kwa upande wa klabu ya Manchester City
,alijiunga na klabu hiyo akitokea Barcelona. Amesaini mkataba mpya mwezi April 2013,na analipwa mshahara wa 200.000£ kwa wiki
10. Sergio Aguero – £24m
Taarifa ni kwa mujibu wa mtandao huu wa Sports4lifetz kushirikiana na Dail mirror na Top10th.com
0 comments:
Post a Comment