Saturday, 24 May 2014

Real Madrid na Athletico Madrid fainali UEFA leo hii

Hii leo kwa mara ya kwanza  katika Historia ya  michuano ya ligi ya mabingwa ulaya UEFA , Timu toka Mji mmoja, Real Madrid na Atletico Madrid,  zitakutana kwenye Fainali huko Lisbon, Ureno.
Hii ni mechi ya watani wa jadi wa Jiji la Madird, ‘EL DERBI MADRILEÑO’, iliyohamia Lisbon.
Mpambano huo unapigwa kuanzia saa 3 dakika 45 usiku Huku kukiwa na wasiwasi kwa kila Timu kuwakosa Mastaa wao kutokana na Majeruhi kwa Real kuhofia kuhusu Cristiano Ronaldo na Atletico kuwa na wasiwasi kwa Diego Costa, kila Timu imezidisha bidii kuwaandaa Mastaa hao.
Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, amedokeza kuwa Ronaldo atakuwa fiti kwa Mechi ya Leo pale alipotamka: “Ronaldo amefanya Mazoezi bila tatizo lakini Pepe na Benzema hawakufanya Mazoezi Wiki nzima na tutaamua kesho [Hii Leo] kama watashiriki.”
Ancelotti pia alisema nia yake ni kutimiza ndoto ya ‘La Decima’ yaani kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya.
Wasiwasi mkubwa upo kwa Diego Costa ambae aliumia Jumapili iliyopita Atletico walipotoka Sare 1-1 na Barcelona huko Nou Camp na kutwaa Ubingwa wa La Liga.
Costa, Mzaliwa wa Brazil ambaye ameamua kuichezea Hispani katika fainali za kombe la dunia, alisafirishwa kwenda Belgrade, Serbia kupata Tiba maalum, Jana alifanya Mazoezi Uwanja wa Estadio da Luz huko Lisbon, na Kocha wa Atletico, Diego Simeone, amesema: “Tutamchunguza Diego na Arda Turan na kutoa uamuzi.”
Ikumbukwe kuwa Atletico wanatinga kwenye Fainali hii ya Ulaya mara tu baada ya Wikiendi iliyopita kutwaa Ubingwa wa Hispania kwa mara ya kwanza tangu Mwaka 1996 lakini hii pia ni Fainali yao ya kwanza ya Ulaya tangu Mwaka 1974 ambako walifungwa na Bayern Munich mabao 4-0 katika Mechi ya Marudiano baada ya kutoka 1-1 katika Mechi ya Kwanza.
Kwa Real Madrid wao wanawania Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10, wenyewe wameubatiza ‘La Decima’, lakini nao hii ni Fainali yao ya kwanza tangu Mwaka 2002 ambapo Zinedine Zidane alifunga Bao la Miujiza na kuwapa Ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Mbabe wa mechi hiyo atakutana na  Sevilla, pia ya Hispania mabingwa wa michuano ya pili kwa ukubwa ya UEFA, Europa League katika mechi ya Super Cup ya UEFA.
Na pia ataingia moja kwa moja Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment