Taifa stars kidedea mbele ya Malawi
Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars bao 1-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Israel Nkongo aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Jesse Erasmo wote wa Tanzania, Taifa Stars ilikwenda mapumziko ikiwa tayari inaongoza kwa bao hilo.
Bao hilo lilifungwa na kiungo mkongwe, Amri Kiemba dakika ya 35 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi nzuri ya mchezaji wa AS Cannes ya Ufaransa, Shomary Kapombe kutoka wingi ya kulia.
Mchezo huu ulikuwa maalum kwa kila timu kujiandaa na mchezo wa marudiano wa hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
Kwa maana hii Stars inashinda mechi ya pili mfululizo nyumbani chini ya kocha mpya, Mholanzi Mart Nooi.
Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi nayo imecheza mechi ya mwisho ya majaribio kabla ya kwenda N’djamena kuikabili Chad.
Tanzania itakuwa ugenini wikiendi hii kujaribu kutafuta nafasi ya kusonga mbele dhidi ya Malawi
0 comments:
Post a Comment