Tuzo za ligi kuu Tanzania Bara Kipre mchezaji bora,Mwambusi kocha bora
WadhaminiI wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, jana walitoa zawadi kwa washindi mbalimbali wa ligi hiyo iliyofikia tamati Aprili 19, mwaka huu.Katika tuzo hizo mchezaji wa Azam FC kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 akiwapiku Anthony Matogolo wa Mbeya City na Lugano Mwangama wa Prisons na amezawadiwa kitita cha Sh. Milioni 5.2.
Huku kipa wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ ameshinda tuzo ya mlinda mlango bora wa Ligi Kuu akiwapiku David Burhan wa Mbeya City na Beno Kakolanya wa Prisons.
Tuzo ya Mfungaji bora wa msimu ilikwenda kwa mshambuliaji wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe, aliyefunga mabao 19 na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.2.
Tambwe aliwashinda Elias Maguri wa Ruvu Shooting, Kipre Tchetce wa Azam FC wote mabao 13, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza wote wa Yanga SC ambao wote walifunga mabao 12 kila mmoja.
Isitoshe,Tuzo ya kocha bora ilikwenda kwa Juma Mwambusi wa Mbeya City, akiwashinda Charles Boniface Mkwasa wa Yanga SC na Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar na kupewa Sh. Milioni 5.2.
Refa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam ameibuka mwamuzi bora akilamba Sh. milioni 7.8 baada ya kuwabwaga Isihaka Shirikisho wa Tanga na Jonasia Rukia wa Kagera walioingia kwenye kipengele hicho.
Vilevile Yanga SC imeibuka timu yenye nidhamu kwa mara nyingine baada ya kutwaa tuzo hiyo pia msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu na kuzawadiwa Sh. Milioni 16 ikizipiku Azam FC na JKT Oljoro.
Zawadi nyingine zilizotolewa ni pamoja na Sh. milioni 75 iliyokwenda kwa Azam FC waliotwaa ubingwa, Yanga SC Sh. milioni 35, Mbeya City Sh. milioni 26 na Simba SC Sh. 21.
0 comments:
Post a Comment