Vijana wa Azam wanatakiwa kambini Mei 25
Uongozi wa Timu ya Azam Fc unawatangazia wachezaji wake wote wa timu ya Vijana kuwa tarehe ya kuripoti kambini ni tarehe 25/06/2014 hii ni kutokana na mabadiliko ya tarehe za Mashindano yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa saba mwishoni,imeelezwa na tovuti ya klabu hiyo
Baada ya mashindano hayo kubadilishiwa ratiba uongozi umefuta tarehe ya awali ya kuripoti kambini ambayo ilikuwa tarehe 08/06/2014.
Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa usaili wa vijana utafanyika Tarehe 01/07/2014 Saa 1. 30 Asubuhi Chamazi.
Usahili huo utahusisha vijana wenye umri wa miaka 15, 16 na 17 tu.
Azam imeeleza kuwa kwa wale Watakaopenda kufika kwenye usaili huu wafike kabla ya Saa 1.00 Asubuhi katika uwanja wa Chamazi.
0 comments:
Post a Comment