Ronaldo amfunika Messi bado kidogo kwa Raul
Mchezaji bora wa dunia na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo Amempita nyota wa Barcelona Lionel Messi katika rekodi za ufungaji mabao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kufunga bao jumamosi hii kwenye fainali ya UCL dhidi ya Athletico Madrid kule Lisbon.Ronaldo mwenye miaka 29 ambaye alibeba tuza ya Ballon d'Or mwezi January kutoka kwa Messi, alifunga bao la nne kwa njia ya pelnati katika ushindi wa mabao 4-1 kule Lisbon.
Ronaldo kwa sasa ameachwa mabao matatu na mchezaji wa zamani wa Madrid Raul, ambaye amefunga mabao 71 katika michezo 144 ya ligi ya mabingwa ulaya.
Mreno huyo hana uwiano mzuri wa kuifungia mabao Madrid kwa sasa amefunga mabao 68 katika michezo 107 huku Messi akifunga mabao 67 katika michezo 86 ya ligi hiyo ya mabingwa ambapo mabingwa wapya kwa msimu huu ni Real Madrid.
Rekodi za ufungaji mabao Uefa
Mchezaji Mabao Michezo
Raul 71 144
Christian Ronaldo 68 107
Messi 67 86
Van Nistelrooy 60 81
Shevchenko 59 116
0 comments:
Post a Comment