Zanetti kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu
Mchezaji Mkabaji wa Inter Milan
na raia wa Argentina Javier Zanetti
alithibitisha jana Jumanne kwamba atastaafu mwishoni mwa msimu baada ya kucheza
mechi 800 kwenye misimu 19 akiwa na klabu hiyo ya Serie A,imeripotiwa na Supersports.com.
“Nilihisi kwamba wakati umefika,”
Zanetti, anayetimiza miaka 41 Agosti na anayesifiwa sana kwamba mchezaji wa
kuigwa, aliambia gazeti la Buenos Aires la La Nacion kwenye mahojiano.
“Soka imenipa mengi sana na
nimefurahia yote.”
Zanetti, aliyechezea taifa lake
mechi 145 licha ya kuachwa nje ya vikosi vya Kombe la Dunia 2006 na 2010 katika
hali ya kutatanisha, alijeruhiwa misuli ya kifundo cha mguu Aprili, jeraha lake
la kwanza kuu katika uchezaji wake. Alipona na kurudi tena uwanjani na kucheza
mechi 10 katika Serie A msimu huu.
Mashabiki wa Inter walikasirika sana
Jumapili kocha Walter Mazzarri alipomuweka benchi muda wote mechi ambayo
walilazwa 1-0 na AC Milan, hatua iliyomnyima nafasi ya kucheza kwenye mchezo wa
watani wa jadi.
“Baada ya jeraha hilo, nilitaka
kuonyesha kwamba ningeweza kurudi na kucheza soka ya ushindani tena. Ninahisi
kwamba sasa niko kamili na nimetimiza yale niliyolenga,” akasema.
Zanetti.
"anastaafu akiwa na miaka 41 na akiwa bado unacheza vizuri ni jambo kuu
sana.,”
Amecheza
kwenye Serie A mechi 613, idadi ambayo imepitishwa tu na mlinzi wa zamani wa AC
Milan Paolo Maldini. Alicheza mara 105 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na jumla ya
mechi alizochezea Inter ni karibu 850. Ameshinda mataji matano ya Serie A,
manne ya Kombe la Italia, pamoja na moja la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, moja la
Kombe la Uefa na moja la Kombe la Dunia la Klabu.
0 comments:
Post a Comment