Wachezaji Brazil waomba tena msamaha,Oscar hana hamu kabisa
Baada ya jana wenyeji kuchapwa mabao 3-0 na Uholanzi katika kumtafuta mshindi wa tatu fainali za kombe la dunia,kwa mara nyingine tena wachezaji wa Brazil wameomba msamaha"Sidhani kama tulistahili kumaliza mashindano kwa mtindo huu,"alisema nahodha Thiago Silva.
"Tunahitaji kuomba msamaha,wametuzomea katika hatua za mwisho,ni kawaida.ni hali ambayo ni ngumu."
Kiungo Oscar ameonekana akikata tamaa moja kwa moja ikiwa ni siku nne tu zimepita baada ya kudhalilishwa na Ujerumani kwa kichapo cha 7-1 katika nusu fainali.
"Nitasema nini,tulikuja hapa na matumaini kibao ya kushinda nafasi ya tatu lakini tumeshindwa," alisema Oscar .
"Tumepoteza mchezo, hakuna cha kuzungumza.aliongeza Oscar
Bao la Robin van Persie liliwapa uongozi Uholanzi dakika ya 3 kabla ya , Daley Blind hajafunga bao la pili dakika ya 13 na Georginio Wijnaldum akafunga la tatu katika muda wa nyongeza dakika 90.
Baadaye leo Ujerumani watacheza na Argentina katika fainali ambayo itaanza saa nne usiku kwa saa za nyumbani.
0 comments:
Post a Comment