Mwenyekiti wa Ferari astaafu baada ya miaka 23.
Mwenyekiti wa Ferrari Luca Di Montezemolo amestaafu kuongoza kampuni hiyo inayojihusisha na langalanga baada ya kuongoza kwa miaka 23.
Di Montezemolo, 67 amesema kuwa baada ya utumishi huo kwa sasa ameamua kuondoka madarakani na anajivunia mafanikio aliyoyapata kwa muda huo.
Sergio Marchionne ndiye atakayechukua mikoba ya Di Montezemolo, ambaye ataanza kazi Octoba 13
Kampuni ya Ferrari haijashinda taji lolote kuanzia mwaka 2008
Katika mashindano yaliyomalizika juzi ya Italia Grand Prix waendesha magari wa Ferari walishika nafasi isiyoridhisha ambapo Fernando Alonso alitangaza kustaafu huku mwenzake Kimi Raikkonen akishika nafasi ya 9.
.

0 comments:
Post a Comment