Tuesday, 27 May 2014

Zawadi za VPL kutolewa leo,Azam kubeba mil 75,Tambwe mil 5.2

Wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, leo inatarajiwa kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali wa ligi hiyo iliyofikia tamati Aprili 19, mwaka huu.
Katika zawadi hizo, bingwa Azam FC atajinyakulia sh milioni 75, mshindi wa pili Yanga sh milioni 37, wa tatu Mbeya City sh milioni 26 na Simba iliyokamata nafasi ya nne itajipoza kwa sh milioni 21.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba pia kutakuwa na zawadi kwa mfungaji bora ambaye ni mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe, atakayelamba sh milioni 5.2, timu yenye nidhamu sh milioni 16, kipa bora sh milioni 5.2 na mwamuzi bora ambaye naye ataondoka na sh milioni 5.2.
Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:00 jioni na kurushwa ‘live’ na Azam TV.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment