Saturday, 7 June 2014

Al Hilal yaanza na sare dhidi ya AS Vita,kesho TP Mazembe na Zamalek

Mashindano ya CAF ya Klabu yamendelea Wikiendi hii, kuanzia jana , kwa Mechi za CAF CHAMPIONZ LIGI na KOMBE la SHIRIKISHO.
Kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI, jana  Al Hilal wakiwa Nyumbani huko Sudan walicheza na AS Vita Club ya Congo DR na kutok sare ya bao 1-1
TP Mazembe, yenye Wachezaji mahiri wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, itakuwa Nyumbani Lubumbashi kuwavaa Wakongwe wa Misri Al Zamalek.
Coton Sport watacheza bila ya Kipa wao Loic Feudjou na Beki Cedric Djeugoue ambao wako na Timu ya Taifa ya Cameroun watakapocheza huko Abidjan dhidi ya ASEC Mimosas.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Leo Jumamosi Juni 7
Entente Sportive de Sétif v Al Ahli - Benghazi
Jumapili Juni 8
TP Mazembe v Al Zamalek
Espérance Sportive de Tunis v Club Sportif Sfaxien
KOMBE LA SHIRIKISHO
Leo Jumamosi Juni 7
ASEC Mimosas Abidjan v Coton Sport FC
E.S. Sahel v Nkana FC Kitwe
Sewe Sport v Al Ahly
AS Real de Bamako v AC Leopards de Dolisie

0 comments:

Post a Comment