Sunday, 8 June 2014

Alex Sanchez awindwa na Manchester United,Lukaku asema anahama kutoka Chelsea.

Nchini Uingereza  kumepambwa taarifa kwamba Manchester United iko njiani kuzipiga vikumbo Liverpool na Tottenham ili kumnasa Staa wa Barcelona Alexis Sanchez.
Mapema kulikuwa na Ripoti kuwa Juventus wametoa Ofa ya Pauni Milioni 16.5 ili kumnunua Sanchez, Straika kutoka Nchini Chile mwenye Miaka 25, lakini Barca haitaki kusikiliza Ofa yeyote chini ya Pauni Milioni 20.
Ujio wa Kocha mpya wa Barca, Luis Enrique, umemweka Sokoni Sanchez na Kocha mpya wa Man United, Louis Van Gaal, anataka kuimarisha Kikosi chake huku ikidokezwa Wachezaji kama Nani na Ashley Young wako njiani kuondoka.
Msimu huu uliokwisha, Sanchez aliifungia Barca mabao 21 wakati mambo kwa  ROMELU LUKAKU ni tofauti yeye amsema kuwa anataka kuihama Chelsea kabla Msimu ujao kuanza.
Kwa Misimu miwili iliyopita, Lukaku, mwenye Miaka 21 na mshambuliaji wa Ubelgiji, amekuwa aking’ara mno kwenye Klabu alizochezea kwa Mkopo, West Bromwich Albion na Everton, lakini inaelekea hata Msimu ujao pia itabidi acheze nje ya Chelsea kwa Mkopo.
Hivi sasa, Chelsea wako njiani kumsaini Straika hatari wa Atletico Madrid na Hispania, Diego Costa, na hilo limemfanya Lukaku ajifikirie.
Lukaku amesema: “Unajua Chelsea kila Mwaka wananunua Straika wa juu. Mwaka Jana niliwaona Samuel Eto'o na Demba Ba na nikjiuliza: ‘'Whoah! Nini kinatokea hapa? Lakini si tatizo. Klabu nyingi zinanitaka. Kwa sasa inabidi nijiangalie mwenyewe. Ni lazima nicheze Kombe la Dunia vizuri. Hilo ni muhimu kwa kila Mchezaji anaetaka Uhamisho na mie ni lazima mmoja wao. Chelsea wanajua nini msimamo wangu!’”

0 comments:

Post a Comment