Sunday, 22 June 2014

Baada ya miaka 16 Hatimaye Nigeria ng'aring'ari,yaishinda Bosnia ya Dzeko

Baada ya miaka 16 ya kutoshinda mchezo wa fainali za kombe la dunia hatimaye Timu ya taifa ya Nigeria  imeonja ladha ya ushindi  kwa kuichapa Bosnia bao 1-0 katika kombe la dunia kundi la  F.
Huu nio ushindi wa kwanza tokea 1998 kwa bao la Peter Odemwingie dakika ya 29 akipokea pasi ya Emmanuel Emenike,na kuipeleka  Nigeria katika nafasi ya pili wakiwa na alama 4 ila  Argentina wana alama 6.

Nigeria itacheza na Argentina  katika mchezo wa mwisho wa makundi siku ya jumatano  na wanahitaji alama ili wafuzu hatua ya mtoano. nafasi ya tatu iko kwa  Iran,  wakiwa na alama moja na Bosnia hawana cha kutafuta kwa sasa.
Ratiba ya leo
JUMAPILI, JUNI 22, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Belgium v Russia
H
Estadio do Maracanã
2200
South Korea v Algeria
H
Estadio Beira-Rio
0100
United States v Portugal
G
Arena Amazonia

0 comments:

Post a Comment