Klose na Ronaldo wameweka rekodi zao mbele ya Ghana kila wakicheza,mhhhh pata uhondo zaidi.
Mchezaji Miroslav Klose wa Ujerumani amesawazisha rekodi iliyokuwa inashikiliwa na nyota wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima ya kufunga mabao 15 katika fainali za kombe la dunia baada ya kuingia akitokea benchi.Mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 ambaye mwaka huu anacheza fainali zake za nne alifunga bao dakika ya 71 na ni bao lake la 69 katika mashindano ya kimataifa.
Klose mfungaji bora wa kombe la dunia mwaka 2006 akiwa na mabao 5 alimaliza akiwa wa pili mwaka 2002 akifunga mabao 5 pia na kule Afrika ya kusini mwaka 2010 alifunga mabao manne.List ya wachezaji waliofunga mabao mengi iko hapo chini.
![]() |
| Klose akiwatoka mabeki wa Ghana. |
Ni wazi kuwa Ronaldo na Klose wameweka rekodi zao mbele ya timu ya Afrika ambayo ni Ghana.



0 comments:
Post a Comment