Breaking news:Fabregas asaini miaka mitano Chelsea
Klabu ya Chelsea ya Uingereza imekamilisha usajili wa kiungo wa Barcelona na mchezaji wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas.Klabu hiyo inayoongozwa na Jose Mourinho imetoa kiasi cha £30 mil kwa ajili ya nyota huyo wa Hispania ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Stamford Bridge.
Fabregas amefunga mabao 8 kwenye La Liga kwa upande wa Barcelona kutengeneza mabao 19 katika msimu huu kwa kucheza michezo 36 na kuushukuru uongozi wa klabu hiyo .
Fabregas mwenye miaka 27 amesema kuwa anawashukuru watu wote ndani ya klabu ya Barcelona baada ya kuitumikia kwa miaka mitatu na kusisitiza kuwa ni klabu yake aliyoichezea tokea utotoni.
"Nilikuwa nahisi kuwa sijamaliza kucheza ligi kuu ya Uingereza,na sasa huu ni muda wa kurudi pale.alisema Fabregas
Fabregas alichezea Arsenal kwa miaka nane kabla ya kurudi tena Barcelona.
0 comments:
Post a Comment