Saturday, 14 June 2014

Uingereza na Italia kumbukumbu ya Euro 2012

Baada ya iIjumaa hii dunia kushuhudia adhabu kubwa ikitolewa kwa Hispania cha mabao 5-1 kutoka kwa Uholanzi na pia Chile kuilaza Australia mabao 3-1 katiika kundi la B hii leo kundi D la Fainali za Kombe la Dunia  zinaanza Mechi zao za kwanza kwa Uruguay kuivaa Costa Rica huko Estadio Castelão Jijini Fortaleza na kufuatia ule Mpambano wenye hisia na kusubiriwa kwa hamu, Uingereza dhidi ya Italia.
Kwa upande wa Uingereza mshambuliaji Danny Welbeck amepona tatizo lake la enka lakini Alex Oxlade-Chamberlain bado hajapona maumivu ya Goti lake aliloumia walipocheza Mechi ya Kirafiki na Ecuador huko Marekani Wiki 2 zilizopita.

Italia huenda wakalazimika kutumia washambuliaji watatu  ilhali walinzi wanne kusimama ukutani na hii imetokea baada ya Mattia De Sciglio kuumia Pajani.
Kuna taarifa njema kuwa  Mario Balotelli na Marco Verratti wamepona matatizo yao kiafya.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa Saba za usiku kuamkia Jumapili.
Uingereza wana kumbukumbu ya kutolewa na Italia kwenye Mashindano ya mwisho makubwa huko kwenye michuano ya EURO 2012 walipotolewa kwa Mikwaju ya Penati.
Kama ilivyokuwa kwenye EURO 2012, aliyetengeneza  mabao kwa Italia ni Mkongwe Andrea Pirlo, ambaye sasa ana Miaka 35, Miaka minne iliyopita alitoa Pasi nyingi kupita Wachezaji wote wa Kiungo wa Uingereza na kuzunguka umbali mrefu kupita Mchezaji yeyote wa Uingereza kwenye Mechi hiyo ya EURO 2012.
 Chini ya Kocha Roy Hodgson timu ya Uingereza  ina wachezaji Chipukizi,Daniel Sturridge, Raheem Sterling na Ross Barkley, wakiongezwa nguvu na Wakongwe Steve Gerrard, Frank Lampard na Wayne Rooney.

Kutokana na Jiji la  Manaus kuhofiwa kuwa na athari za Joto,timu zote mbili zitacheza Soka la tahadhari la kumiliki Mpira ili wasiupoteze ovyo na kupoteza nguvu kwa kuukimbiza kutaka kuumiliki tena.

0 comments:

Post a Comment