Hatimaye Wambura arudishwa na TFF kugombea Urais wa Simba Juni 29
![]() |
Michael Wambura |
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya mchana wa leo ofisi za TFF,Dar es Salaam,na kusema kuwa Wambura amerudishwa baada ya kikao chao kilichodumu kwa siku mbili.
Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumtoa katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Juni 29 2014.
Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.
Kwa maana hiyo Wambura sasa atachuana na Evans Aveva pamoja na Andrew Tupa.
0 comments:
Post a Comment