List Wanaoongoza kufunga mabao Mengi kombe la dunia,Ronaldo anaweza kupitwa iwapo Klose akifunga mawili tu
![]() |
Ronaldo de Lima |
Ronaldo alicheza kombe la dunia miaka ya 1998, 2002 na 2006.
Sport4lifetz inakuletea kumi bora ya wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi,Anayemfuata kwa karibu ana mabao 14 , ni Miroslav Klose mwenye miaka 36 wa Ujerumani sambamba na mjerumani mwenzake ambaye hachezi soka kwa sasa Gerd Muller,.
Mchezaji/Nchi | Mabao |
Ronaldo-Brazil | 15 |
Miroslav Klose-Ujerumani | 14 |
Gerd Muller-Ujerumani | 14 |
Just Fontaine-Ufaransa | 13 |
Pele-Brazil | 12 |
Sandor Kocsis-Hungary | 11 |
Jurgen Klinsmann-Ujerumani | 11 |
Helmut Rahn-Ujerumani | 10 |
Gary Lineker-uingereza | 10 |
Gabriel Batistuta-Argentina | 10 |
Nyota wa zamani wa Ufaransa aliyecheza soka miaka ya 1958 Just Fontaine - amefunga mabao 13 .
Akiwa na mabao 12 katika mashindano nne ya kombe la dunia kuanzia 1958 na 1970, gwiji wa Brazil Pele ni nyota kwenye nchi yake akiwa na mabao hayo na kubeba kombe mara 3
Wachezaji wawili wamefunga mabao 11 kila moja , gwiji wa Hungary Sandor Kocsis na Mjerumani Jurgen Klinsmann.
Kumi bora inafungwa na Mjerumani , Helmut Rahn, mwaka wa 1954 na 1958, mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Gary Lineker pamoja na Muarjentina, Gabriel Batistuta.
Iwapo mwaka huu David Villa wa Hispania (mabao 8) au Diego Forlan wa Uruguay (mabao ) wakifunga mabao mengi mwaka huu kule Brazil wanaweza wakaingia kwenye list.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Sports4lifetz kushirikiana na Goal.com
0 comments:
Post a Comment