Thursday, 19 June 2014

Hispania,Cameroon na Australia kwaherini kombe la dunia

Mabingwa  wa Dunia Hispania Jana huko Estadio do Maracanã Jijini Rio de Janeiro Nchini Brazil walinyukwa mabao 2-0 na Chile na kuvuliwa Ubingwa wa Dunia na kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huku wakiwa wamebakisha Mechi moja ya Kundi B dhidi ya Australia ambao nao wametupwa nje.
Hispania, ambao walitandikwa mabao 5-1 Uholanzia kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi B, Jana walifungwa mabao yote mawili katika Kipindi cha Kwanza mabao yalifungwa na Eduardo Vargas na Charles Aranguiz.
Hispania wamekuwa Mabingwa wa kwanza wa  Dunia kutupwa nje kwenye kabla kutinga Raundi ya Kwanza ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Dunia.
Matokeo mengine  huko Arena Amazonia Jijini Manaus Nchini Brazil, Croatia imewafunga Cameroon mabao 4-0 kwenye Mechi ya Kundi A la Fainali za Kombe la Dunia na kuitupa nje ya Mashindano haya.
Cameroon, wakiwa wamebakisha Mechi moja ya Kundi A dhidi ya Wenyeji Brazil, wanaungana na Hispania na Australia kuyaaga Mashindao haya.
Lakini Uholanzi imechungulia Raundi ya Pili  baada ya kuichapa Australia mabao 3-2 kwenye Mechi ya Kundi B iliyochezwa Estadio Beira-Rio Mjini Porto Alegre Nchini Brazil.
Uholanzi walitangulia kwa Bao la Arjen Robben ambalo lilidumu Dakika 1 tu na Tim Cahill kusawazisha na kisha Australia kwenda mbele mabao 2-1 Kipindi cha Pili kwa Penati ya Mile Jedinak.
Lakini Uholanzi walisawazisha Dakika 4 baadae kupitia Nahodha wao Robin van Persie na kupata ushindi kwa Bao la Memphis Depay.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Uholanzi na  kipigo cha pili mfululizo kwa Australia ambao walichapwa 3-1 na Chile kwenye Mechi ya Kwanza.
 Mechi za leo
ALHAMISI, JUNI 19, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Colombia v Ivory Coast
C
Nacional
2200
Uruguay v Uingereza
D
Arena Corinthians
0100
Japan v Ugiriki
C
Estadio das Dunas

0 comments:

Post a Comment