Hatima ya Wambura kwa mara ya pili kujulikan leo
KAMATI ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inatarajiwa kukutana leo mchana kupitia rufaa ya mgombea wa nafasi ya urais wa klabu ya Simba, Michael Wambura, anayepinga kuenguliwa kwa mara ya pili.Wambura aliwasilisha rufaa kwa mara ya pili jana, baada ya Jumatatu iliyopita Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake Dk. Damas Ndumbaro kumuengua kwa madai ya kufanya kampeni kabla ya muda.
Akizungumzia hilo jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Julius Lugaziya, alisema kamati yake itakaa leo saa 8 mchana kupitia rufaa hiyo.
Uchaguzi wa Simba unatarajia kufanyika Juni 29 kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ingawa hivi karibuni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa rais Jamal Malinzi lilitangaza kuusitisha.
0 comments:
Post a Comment