Sunday, 15 June 2014

Ivorycoast waanza vema kombe la dunia.

Mabao mawili ya vichwa katika kipindi cha pili ya  Wilfried Bony na Gervinho yameipa ushindi  Ivory Coast au  Cote d'Ivoire kutoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Japan muda mfupi uliopita mechi ya kundi la Group C uwanja wa  Pernambuco huko  Recife,Brazil.

Keisuke Honda  aliwapa uongozi vijana wa  Alberto Zaccheroni baada ya kufunga bao zuri akikokota mpira kwenye boksi kabla ya kufunga..

Vijana wa  Sabri Lamouchi ambaye ni kocha mdogo kuliko wote katika mashindano ya mwaka huu walipwaya kipindi cha kwanza kabla ya kuigia kwa  Didier Drogba katika kipindi cha pili.
Ivory coast inakuwa timu ya kwanza kushinda kutoka Afrika baada ya Cameroon kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mexico.
Ratiba ya leo.muda kwa saa za Tanzania
JUMAPILI, JUNI 15, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Switzerland v Ecuador
E
Nacional
2200
France v Honduras
E
Estadio Beira-Rio
0100
Argentina v Bosnia-Herzegovina
F
Estadio do Maracanã

0 comments:

Post a Comment