Sunday, 15 June 2014

Uingereza yaanza kwa kichapo kombe la dunia

Timu ya taifa ya Uingereza imechapwa  mabao 2-1na Italia katika mchezo wa Kundi D Kombe la Dunia  mapema usiku wa kuamkia leo mjini Manaus.
mchezaji Claudio Marchisio alianza kuifungia Italia dakika ya 35 kabla ya Daniel Sturridge kusawazisha dakika mbili baadaye akimalizia krosi nzui ya Wayne Rooney.
Mchezaji mtukutu Mario Balotelli aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Uingereza, ndiye aliyeifungia bao la ushindi Italia dakika ya 50.

0 comments:

Post a Comment