Tuesday, 24 June 2014

Kampeni uchaguzi Simba zaanza kurindima leo

KAMATI ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba, jana imetangaza orodha ya mwisho ya majina ya wagombea ambao wameruhusiwa kuanza kampeni za kunadi sera zao kwa wanachama kuelekea uchaguzi mkuu wa Juni 29.
Kampeni hizo zinaanza leo na zitafikia tamati Juni 28 saa sita usiku.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba, Dk. Damas Ndumbaro, aliwataja wagombea hao kuwa ni Amina Poyo, Asha Muhaji na Jasmine Badour wanaowania nafasi moja ya ujumbe kwa wanawake.
Nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji wamepita wagombea 18 ambao ni Said Tully, Yasini Mwete, Ally Suru, Rodney Chiduo, Said Pamba, Ally Chaurembo, Abdulhamid Mshangama, Chano Almasi, Damian Manembe, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Kajuna Noor, Hamis Mkoma, Alfred Elia, Said Kubenea, Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid Abdallah na Collin Frisch.
Nafasi ya Makamu wa Rais wapo Bundala Kabulwa, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Swedi Mkwabi na nafasi ya rais inagombewa na Andrew Tupa na Evans Aveva.
Alisema kuna wagombea ambao wana dosari za kimaadili, ambao shauri lao limepelekwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutokana na klabu hiyo kukosa Kamati ya Maadili ambayo ingeweza kusikiliza madai hayo.
“Siku zote mtuhumiwa sio mkosaji, kutokana na sisi hatuna Kamati ya Maadili, makosa yao yatasikilizwa Fifa na uongozi mpya ukiingia madarakani utateua Kamati ya Maadili, endapo Fifa wakiwa bado hawajajibu hilo, litarudi tena kwenye kamati hiyo mpya na kama itatokea kiongozi aliyeingia madarakani atakuwa na mapungufu ya kimaadili atavuliwa wadhifa huo,” alisema.

0 comments:

Post a Comment